Articles by "HABARI ZA BIASHARA"
Showing posts with label HABARI ZA BIASHARA. Show all posts
Mkuu wa kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali wa Benki ya Exim Bw. Silas Matoi, akizungumza na mmoja wa washindi wakati wa droo ya kwanza ya kampeni ya Chanja Kijanja, Dili ndio Hili iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Kupitia kampeni hii, wateja wanaotumia kadi za Exim kulipia bidhaa au huduma wanapata nafasi ya kushinda zawadi ya pesa taslimu TZS 100,000 kila wiki, TZS 200,000 kila mwezi, pamoja na zawadi kubwa za TZS milioni 15, milioni 10 na milioni 5 mwisho wa kampeni.Kushoto ni Meneja Msaidizi wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali wa Benki ya Exim Benedict Mwinula, pamoja na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Rodgers Biteko (kulia), jijini Dar es Salaam.
Droo ya kwanza ya kampeni ya Chanja Kijanja, Dili ndio Hili imeibua washindi watano wa Sh. 100,000 kila mmoja! Mkuu wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali wa Benki ya Exim, Bw. Silas Matoi, aliwatangaza washindi huku akisisitiza kuwa hii ni mwanzo tu.

“Kila wiki, washindi watatangazwa, na kila mwezi washindi 10 watashinda Sh. 200,000. Vilevile, washindi wa droo kuu watapokea zawadi kubwa za Sh. milioni 5, milioni10, na mshindi mkuu Sh. milioni 15,” alisema Bw. Matoi.
Benedict Mwinula, Meneja Msaidizi wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali, pamoja na Rodgers Biteko, Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, walishiriki katika droo hii iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Kampeni ya Chanja Kijanja inalenga kuwapa wateja wa Exim fursa ya kushinda kila wanapotumia kadi za Exim kulipia bidhaa au huduma. Hii ni nafasi yako ya kuwa mmojawapo wa mshindi wa Sh. 15 milioni!

  
Dar es Salaam – Katika hafla ya Marketers Night Out iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa, aliwasilisha mada iliyoangazia kwa kina mchango wa programu ya Imbeju katika kubadilisha maisha ya wananchi, hasa wanawake na vijana, kupitia uwezeshaji wa kiuchumi na kukuza ujumuishi wa kifedha nchini.

Akizungumza mbele ya wataalamu wa masoko, viongozi wa taasisi, wajasiriamali na wadau wa maendeleo, Mwambapa alisema Imbeju ni zaidi ya mpango wa kutoa mikopo pekee bali ni programu jumuishi inayolenga kujenga msingi imara wa ujasiriamali. Alieleza kuwa programu hiyo imejengwa juu ya nguzo tatu kuu; elimu ya ujasiriamali na uongozi, upatikanaji wa mitaji rafiki, pamoja na uunganishaji wa wajasiriamali na masoko pamoja na huduma rasmi za kifedha.
 
“Kupitia mafunzo ya vitendo, washiriki huwezeshwa kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi, kutumia fursa za teknolojia, kufuatilia mapato na faida kwa weledi na kufanya maamuzi sahihi ya uwekezaji. mbinu hiyo imewezesha wajasiriamali wengi kuimarisha biashara zao na kuongeza ajira katika jamii”, alisema Mwambapa

Akizungumzia wanawake, Mwambapa alieleza kuwa wamekuwa walengwa muhimu wa programu kwani ndio mhimili wa ustawi wa familia na jamii. Wanawake wengi waliokuwa wakikabiliwa na changamoto za mtaji na elimu ya ujasiriamali sasa wameweza kuanzisha au kupanua biashara zao kupitia Imbeju, jambo lililosababisha kuongezeka kwa uzalishaji, kuboreshwa kwa kipato cha kaya na kuinuka kwa hali ya maisha ya familia zao. Alisisitiza kuwa uwekezaji kwa mwanamke mmoja hupelekea kuleta mafanikio kwa kizazi kizima.

Kwa upande wa vijana, alisema programu hiyo imekuwa chachu ya kubadilisha fikra bunifu kuwa miradi halisi katika maeneo ya teknolojia, kilimo-biashara, sanaa na biashara mtandao. Kupitia ushauri wa kitaalmu, mafunzo na ufadhili wa mawazo bunifu, vijana wengi wamepata uwezo wa kuzifikisha bidhaa zao katika masoko mengi zaidi kupitia majukwaa ya kidijitali, hivyo kuongeza ushindani na kupanua wigo wa biashara zao.
Mwambapa pia aligusia mchango wa Imbeju katika kukuza ujumuishi wa kifedha nchini kwa kuwawezesha wananchi waliokuwa nje ya mfumo rasmi wa benki kufungua akaunti, kujiwekea akiba, kukopa na kufanya miamala kwa urahisi zaidi baada ya kupata elimu ya kifedha. Kupitia ushirikiano wa CRDB Bank Foundation na Benki ya CRDB, huduma hizi sasa zimefika hata maeneo ya vijijini ambako upatikanaji wa huduma za kifedha ulikuwa mdogo awali.

Alisema hatua hiyo imeimarisha uthabiti wa biashara ndogondogo, kuongeza uwezo wa kujitegemea kwa wananchi na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

Akihitimisha mada yake, Mwambapa alitoa wito kwa wadau wote kuendelea kuwekeza katika mipango inayowawezesha wanawake na vijana, akisisitiza kuwa mafanikio ya Imbeju ni ushahidi kuwa uwekezaji katika watu ndiyo msingi wa kujenga uchumi jumuishi, thabiti na wenye tija kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhi Tuzo maalumu Meneja Mkazi wa Kampuni ya Emirates Leisure Retail Zanzibar, Paul Atallah (wa pili kushoto), kwa niaba ya kampuni hiyo na Qatar Foundation kwa kutambua mchango wao mkubwa katika kusaidia watu wenye uhitaji.

Na Dotto Mwaibale, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa Tuzo maalum kwa Kampuni ya Emirates Leisure Retail Zanzibar na Qatar Foundation kwa kutambua mchango wao mkubwa katika kusaidia watu wenye uhitaji.

Dkt. Mwinyi alitoa tuzo hizo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu yaliyofanyika Desemba 4, 2025 kwenye Ukumbi wa Dr. Shein – Tunguu, Chuo Kikuu cha SUZA, Mkoa wa Kusini Unguja tukio lililohudhuriwa na viongozi wa Serikali, wadau wa maendeleo, mashirika ya kijamii, na wananchi kutoka sehemu mbalimbali za Zanzibar.

Akihutubia katika maadhimisho hayo Rais Mwinyi aliwataka wadau kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwawezesha watu wenye ulemavu na alisisitiza kuwa maendeleo ya kweli ni yale yanayowahusisha watu wote bila kuacha kundi lolote nyuma.

Aidha, Dkt. Mwinyi alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wadau na wahisani kwa kujitolea kwao kuchangia maendeleo ya jamii zenye watu wenye ulemavu na kueleza kuwa Serikali itayafanyia kazi maoni na ushauri uliotolewa ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata fursa kamili za kutimiza malengo yao.

Kwa upande wake Meneja Mkazi wa Kampuni ya Emirates Leisure Retail Zanzibar, Paul Atallah, alilishukuru Baraza la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar kwa kutambua mchango wa Emirates Leisure Retail na kueleza kwamba kampuni hiyo itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Serikali na jamii katika kuleta maendeleo chanya kwa watu wenye ulemavu.

Utambuzi wa Wadau Maalumu

Katibu Mtendaji wa Baraza la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar, Ussi Khamis Debe, akizungumza kwenye maadhimisho hayo alitoa shukrani kwa wadau wote wanaounga mkono juhudi za Serikali katika kusaidia watu wenye ulemavu.

Aidha, kwa nafasi ya kipekee alimshukuru Afisa Utawala Msaidizi wa Kampuni ya Emirates Leisure Retail Zanzibar, Ramadhan Hussein Layya (Maarufu Msokolo),kwa mchango wake mkubwa na wa muda mrefu, hususan katika kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi kupitia misaada, ushiriki, na michango inayobadilisha maisha ya wanufaika.

Kaulimbiu ya Maadhimisho:

"Uwezeshaji na Ushirikishwaji wa Watu Wenye Ulemavu kwa Maendeleo Jumuishi."

Misaada Iliyotolewa katika maadhimisho hayo kwa ajili ya makundi mbalimbali ya wahitaji ni

Vyerehani kwa ajili ya kujiajiri, kofia maalumu (round hats) kwa ulinzi wa ngozi, miwani ya kinga na vifaa vya kurekebisha uoni, baiskeli za mwendo kwa watu wenye ulemavu wa viungo, fedha za mikopo kwa kuanzisha au kuendeleza biashara.

Vifaa vingine vilivyotolewa ni vya kuongeza uwezo wa kujitegemea mashine za kusaga nafaka.

Misaada hiyo imeleta furaha, matumaini, na thamani kubwa kwa wanufaika na familia zao, ambayo inakwenda kuwasaidia kutimiza ndoto zao na kuimarisha ustawi wa familia zenye watu wenye uhitaji maalumu.

Kauli ya Emirates Leisure Retail Zanzibar na Qatar Foundation:

Uongozi wa kampuni hizo umeeleza dhamira zao za kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine kuhakikisha watu wenye ulemavu Zanzibar wanapata fursa sawa za ustawi na maendeleo, na kuendelea kuwekeza katika miradi ya kijamii inayobadilisha maisha ya watu wenye uhitaji maalumu.
Viongozi wa Kampuni hizo na wadau mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

Dar es Salaam, 30 Novemba 2025: Dhamira ya PUMA Energy Tanzania ya kutoa ubora, ubunifu na huduma yenye kujikita kwa mteja, imethibitishwa kwa matokeo chanya. Usiku wa jana kwenye hafla ya mwaka ya Consumer Choice Awards, baada ya kutunukiwa tuzo mbili kubwa zaidi za usiku huo ambazo ni “Kampuni Inayopendwa Zaidi ya Mafuta na Nishati Barani Afrika” na “Kituo cha Mafuta kinachotoa Huduma kwa Wepesi na Kupatikana kwa urahisi.”

Ushindi huu wa tuzo mbili unaonesha kwamba PUMA Energy si tu kinara katika huduma za rejareja za nishati hapa Tanzania, bali pia katika bara zima la Afrika. Tuzo hizi, zilizopigiwa kura na watumiaji pamoja na wataalamu wa sekta, ni uthibitisho wa mkakati wa kampuni katika kutoa bidhaa bora za mafuta na nishati, mtandao mpana wa vituo vya kisasa, na kiwango cha juu cha utoaji wa huduma.
Tuzo ya “Kampuni Inayopendwa Zaidi ya Mafuta na Nishati Barani Afrika” ni uthibitisho wa taswira chanya ya PUMA Energy barani kote Afrika na picha ya uaminifu, weledi wa kiutendaji, na suluhu bunifu za nishati. Tuzo hii inaonyesha imani ambayo mamilioni ya watumiaji, wafanya biashara, na washirika wanaendelea kuwa nayo kwa PUMA Energy katika shughuli zao za kila siku.

Wakati huo huo, tuzo ya “Kituo cha Mafuta kinachotoa Huduma kwa Wepesi na Kupatikana kwa urahisi.” inaonesha ubora wa utekelezaji wa kampuni hapa nchini. PUMA Energy imewekeza kwa uthabiti kwenye maeneo ya kimkakati, miundombinu ya kisasa, na huduma zinazokidhi mahitaji ya madereva wa kisasa wa Kitanzania kuanzia vituo vyenye mwanga wa kutosha, usalama, usafi wa mazingira, malipo ya kidigitali, hadi mtandao mpana unaohakikisha kituo cha PUMA hakiko mbali na mteja.
Mkurugenzi Mtendaji wa PUMA Energy Tanzania, Fatma Abdallah, alisema:Tunapenda kurudisha shukrani zetu kwa wateja na watumiaji wetu, kwa kutupa sisi nafasi ya kupokea tuzo hizi kubwa. Tuzo hii ya Kampuni inayopendwa zaidi ni mafanikio makubwa yaliyochangiwa na kila mshiriki wa timu ya Puma Enenrgy Tanzania, wauzaji wetu, na wateja wetu wapedwa. Na Tuzo ya Kituo Kinachopatikana kwa Urahisi ni uthibitisho wa kujitoa kwetu na kuhakikisha kila mteja anayeingia kwenye vituo vyetu anapa huduma bila usumbufu, bidhaa za uhakika na kuondoka akifurahi. Tuzo hizi si mwisho wetu, bali zimekuwa chachu ya kutusukuma kuendelea kutoa huduma za viwango vya juu zaidi”

Mwisho, Mkuu wa Sheria na Masuala ya Ushirika wa PUMA Energy Tanzania, Emmanuel G. Bakilana, alisema, “Tunajitahidi kila mara kuhakikisha mteja yupo katikati ya kila tunachofanya.”
Mkuu wa Kanda ya Kati wa Vodacom Tanzania PLC, Chiha Nchimbi (wa pili kushoto), akikabidhi kapu la zawadi kwa Rehema Sangaya, mkazi wa Hombolo, Dodoma (wa tatu kushoto), ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za msimu wa Sikukuu. Tukio hilo limefanyika jijini Dodoma jana, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Vodacom kurejesha kwa jamii na kusherehekea wateja katika kipindi hiki cha sikukuu.

Wanaoshuhudia tukio hilo ni pamoja na Meneja Mauzo wa kampuni hiyo wilayani Kondoa Balikulije Mchome, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkoyo Julius Magawa (wa pili kulia) na Mtendaji wa Mtaa wa Mkoyo, Pendo Mwijalubi (kushoto).

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Benki ya Exim Tanzania imezindua kampeni kubwa ya matumizi ya kadi katika msimu wa sikukuu, iitwayo “Chanja Kijanja, Dili Ndio Hili,” ambayo itadumu kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia 1 Desemba 2025 hadi 31 Januari 2026. Kampeni hiyo inalenga kuhamasisha Watanzania kupunguza matumizi ya fedha taslimu na kujenga utamaduni wa kufanya malipo ya kidijitali, hususan kwa wateja wanaotumia kadi za Exim Mastercard.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo, alisema kampeni hiyo imeandaliwa ili kutoa suluhisho la malipo lililo rahisi, salama na lenye manufaa kwa wateja katika kipindi ambacho matumizi ya ununuzi huongezeka kutokana na sikukuu.

“Lengo ni kufanya malipo ya kila siku kuwa mepesi zaidi na kuwapa wateja nafasi ya kujishindia zawadi kemkem. Hii inaendana na dhamira ya benki katika kukuza matumizi ya malipo ya kidijitali nchini,” alisema.

Katika kipindi cha kampeni, wateja watakaofanya malipo kwa kutumia kadi za Exim Mastercard kupitia mashine za POS au mtandaoni watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali, ikiwemo:

●Zawadi za kila wiki: TZS 100,000 kwa washindi watano (5).

●Zawadi za kila mwezi: TZS 200,000 kwa washindi kumi (10).

●Cashback maalum katika siku za Black Friday (28 Nov 2025), Cyber Monday (1 Des 2025), na Krismasi (25 Des 2025).

●Zawadi kubwa mwishoni mwa kampeni: TZS milioni 5, TZS milioni 10 na zawadi kuu ya TZS milioni 15.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mifumo Mbadala na Mabadiliko ya Kidijitali wa Exim, Silas Mtoi, alisema kampeni hii ni hatua muhimu katika safari ya taifa kuelekea uchumi unaotumia malipo ya kidijitali.

“Mteja akitumia kadi dukani au mtandaoni anapata usalama, kasi na urahisi. Tunataka kuchochea matumizi ya malipo ya kisasa na kupunguza utegemezi wa fedha taslimu nchini,” alisema Mtoi.

Wateja wa Exim pia watanufaika na zawadi na punguzo maalum katika maduka ya Shoppers na Village Supermarket, pamoja na ofa maalum kwenye migahawa na maeneo ya burudani, ikiwemo Karambezi Café na CIP Lounge katika uwanja wa ndege.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Stanley Kafu, alisema kampeni hii imeundwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wateja katika msimu wa sikukuu.

“Iwe ni maandalizi ya sherehe, safari, kununua mahitaji ya familia au kulipia ada za shule, malipo kwa kutumia kadi ya Exim yanampa mteja urahisi, usalama na nafasi zaidi ya kushinda,” alisema.

Aliongeza kuwa kampeni hii ni sehemu ya mkakati wa Exim katika kuharakisha mabadiliko ya kidijitali nchini.

Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania aliipongeza Benki ya Exim kwa kuendesha kampeni inayoakisi uwazi, ukweli na maslahi ya wateja. Aliahidi kuwa droo zote za washindi zitasimamiwa kwa uadilifu na bila upendeleo.

Kwa mujibu wa Exim, ongezeko la matumizi ya kadi litasaidia kupunguza hatari za kubeba fedha taslimu na kuimarisha mfumo wa kifedha wenye ufanisi zaidi. Benki hiyo imewataka wateja wote kushiriki na kufurahia msimu wa sikukuu kupitia kampeni hii.

Kampeni ya “Chanja Kijanja, Dili Ndio Hili” inatarajiwa kuvutia maelfu ya washiriki huku ikibadilisha namna Watanzania wanavyofanya malipo katika msimu wa sikukuu na hata baada ya msimu huo.

Na Mwandishi Wetu, Mtwara

Benki ya Exim imejitokeza kuwa mdhamini mkuu wa mbio za Kilomita 5 katika msimu wa nne wa Korosho Marathon, tukio kubwa la michezo lililofanyika mkoani Mtwara likilenga kuhamasisha afya, ustawi wa vijana na mshikamano wa jamii.

Akizungumza wakati wa mbio hizo, mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Vijana, Mheshimiwa Joeli Nanauka, alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wadau mbalimbali katika kukuza afya na maendeleo ya kijamii kupitia michezo. Alisema kuwa michezo ni nyenzo muhimu katika kuibua vipaji, kujenga umoja na kuongeza ushiriki wa vijana katika shughuli chanya za maendeleo.
“Tunazo fursa nyingi kupitia michezo—si tu kuongeza afya zetu, bali pia kujenga mahusiano bora na kuimarisha mshikamano wa kijamii. Tunapongeza Exim kwa kuonesha mfano wa kujitoa katika kuunga mkono juhudi hizi,” alisema Waziri

Kwa upande wake, Exim Bank ilieleza kuwa udhamini huo ni sehemu ya nafasi yake ya kuchangia maendeleo ya jamii na kuunga mkono shughuli zinazowagusa wananchi moja kwa moja. Benki hiyo imerejea dhamira yake ya kuendelea kushiriki miradi yenye manufaa kwa jamii, ikisisitiza kuwa michezo ni jukwaa muhimu katika kuhamasisha maisha bora, kukuza vipaji na kuimarisha umoja wa wananchi.
Kampuni ya Bima ya SanlamAllianz imewashukuru mawakala wao kwa kufanya kazi nao

Akizungumza wakati wa halfa ambayo imefanyika Novemba, 28,2925 jijini Dar-es-Salaam, Meneja mkuu wa biashara na mawakala, Geofray Masige amesema kuwa kampuni hiyo ya SanlamAllianz wanawashukuru mawakala wake kwa mchango mkubwa walioufanya katika kukuza biashara ya bima.

Pia naenda kuchukua nafasi hii kuwatambulisha mawakala watu juu ya muunganiko wetu mpya wa Sanlam na Allianz.
"Mnamo Septemba 2023, kampuni ya Sanlam bingwa wa huduma za bima barani Afrika na Allianz ambao ni miongoni mwa makampuni makubwa zaidi ya bima duniani ziliungana kutengeneza kampuni kubwa ya kifedha isiyo ya kibenki barani Afrika, inayojulikana kama SanlamAllianz.

Hadi sasa, SanlamAllianz ipo katika nchi 26 barani Afrika.

"Muungano huu umeunganisha uzoefu wa pamoja wa zaidi ya miaka 200 barani Afrika na duniani.
Malengo yetu ni kutoa huduma bora zaidi, kuunda bidhaa zinazokidhi matarajio ya wateja, na kujenga jamii inayopata ulinzi wa maisha, fedha, mali, na mafanikio endelevu.

Na hapa ndipo inapotoka kauli mbiu yetu: “Ishi kwa Kujiamini” – Live with Confidence.

Kwa wale old school, sio ile ya kina Msondo na Sikinde hapa tunazungumzia zama za James Bond na Titanic.

"Kufuatia uzinduzi rasmi wa chapa yetu mpya mwishoni mwa mwezi wa kumi, Sanlam General Insurance imeungana na Jubilee General Insurance kuunda SanlamAllianz General Insurance Tanzania.

Vilevile, Sanlam Life Insurance imebadili jina na kuwa SanlamAllianz Life Tanzania.
"Kazi kubwa iliyofanywa na wafanyakazi wenzangu hapa nchini pamoja na wenzetu wa SanlamAllianz Group imetuwezesha kushiriki kikamilifu mabadiliko haya muhimu.

Kwa mujibu wa takwimu za soko la bima nchini.

SanlamAllianz Life inaendelea kuwa kinara katika bima za maisha.

SanlamAllianz General inaelekea kuwa kampuni inayoongoza katika bima za mali kufikia mwisho wa mwaka 2025.

Kwa upande wa General Insurance, tumenufaika sana kupitia muunganiko wa Jubilee Allianz na Sanlam General.

Wafanyakazi wote wanaendelea na majukumu yao kama kawaida, uwezo wetu wa kuandikisha bima (underwriting capacity) umeongezeka, na sasa tunapata utaalamu wa kimataifa kutoka SanlamAllianz Group.

"Hii ni fursa muhimu kwa ukuaji wa soko la bima nchini na pia kwenu ninyi mawakala wetu kwa kuwa ninyi ni sehemu muhimu ya mafanikio haya.

Kwa sasa, SanlamAllianz General Insurance ina takribani mawakala 300 nchi nzima, na lengo letu ni kufikia mawakala 350 ifikapo mwaka 2026.

Mimi na ninyi ni sehemu ya familia hii kubwa ya mawakala wa SanlamAllianz. Mfululizo wa matukio kama haya utafanyika katika matawi yetu yote makubwa ili kila wakala apate nafasi ya kushiriki, amesema,"Masige.

Pia amesema Wana mtandao wa matawi 11, ikiwemo jijini la Mwanza, Arusha, Dodoma, Morogoro, Mbeya, Zanzibar, Moshi, Tanga, Mbagala, Quality Center na Tegeta.